#premierepro#beginner#premierepro#tutorial Adobe Swahili—- Import media

Hujambo mtazamaji popote ulipo na karibu kwa mafunzo ya Adobe swahili ili ujifunze jinsi ya kufanya kazi na program zote za Adobe Creative Cloud 2020.
Leo tutajifunza jinsi ya kuhariri clips kwenye Adobe premiere pro cc kwa kutumia mbinu ya uhariri iitwayo Three-point edits

Kwa hii tutorial natumia editing workspace, unaweza reset workspace kwa ku double click kwenye jina la ku edit kwenye workspace panel kisha ubonyeze yes kwa kuhakikisha.

Unapo edit clips ndani ya sequence siku zote kutakuwa na alama nne kwa wakati ambazo ni muhimu; hizi ni in points mbili na out points mbili.
Hizi huanzisha mwanzo na mwisho wa sehemu ya clip unayotaka kutumia na kuanza na mwisho kwa uwekaji wa hiyo clip kwenye sequence.
Inawezekana kufanya fourth point kutoka kwa nyingine yoyote kati ya hizo tatu.
Kwa hivyo unahitaji points tatu tu na karibu kila wakati clip inaongezwa kwa sequence, inatumia three-point edit.

Wacha tujaribu hii. Nitaenda kufungua assets zangu na nipate butterfly clip kwenye project panel yangu na nita drag kitu chochote katika sequence yangu.

Vizuri, hiyo inafanya kazi kikamilifu, lakini sio three point edit yenyewe. Alama yoyote katika sequence inapuuzwa na kwa kweli sijaelezea kama ni in ama ni outpoint kwenye source clip.

Kwa hivyo naenda kuitoa na control z hapa kwenye windows au command z kwenye mac os.

Sasa katika source monitor, ninayo play head imelingana na pahali ambapo ningependa iwe inpoint, kwa hivyo nitaclick kuongeza moja ya hizo na kisha nadhani labda kama vile butterfly wings ziko karibu na edge ya screen, nitamark outpoint.

Ndani ya timeline panel nitaongeza in point pekee. nitaweka playhead yangu pahali ambapo ninataka na nita press I key kuashiria in point na nitasongeza play head kando.

Sasa ikiwa huna in point, play head itatumika kama in point.
Lakini nataka uone njia ndefu pande zote ili uelewa kikamilifu hii work flow kwanza kabisa.

Tunazo points zetu tatu, tuko tayari kutengeneza edit. Kwa hivyo naenda kubonyeza ili kufanya overwrite edit.

In point iliyoko kwenye source clip imelingana na in point kwenye sequence.

Na tuko na muda wa source clip kama inavyofafanuliwa na hii outmark ambayo imeongezwa kwenye sequence.

Na fourth point imekua calculated automatically kwenye sequence kulingana na muda wa source clip.

Unaweza ondoa mojawapo ya four points. Kwa mfano,naenda kuondoa tena na tena ili niondoe marks kwenye timeline panel
na nitaenda ku mark outpoint kwa kubonyeza O key na tena nitasongesha play head kando.

Sasa ninapofanya overwrite edit yangu, mwisho wa clip imekua imelingana na mwisho wa selection kwenye timeline panel.

Ikiwa nitarudisha play head nyuma kidogo, unaweza ona tuko hapo mwisho wa tukio, hii ni nzuri ikiwa una kipande cha clip ambacho mwisho wake ndio muhimu kuliko mwianzo, bado unaweza kuitime kulingana na matukio kwenye sequence.

Japo kuwa hutapata matokeo sawa ikiwa unafanya insert edit ambapo kila kitu kinashuffle out of the way.
Kwa hivyo kutumia mbinu hii wakati wa action hakikisha unatumia ovewrite edit.

Nitaondoa tena na tena. Sasa nitafunga pengo kidogo, nitaenda ku trim mwisho wa hii first clip ili tuwe na nafasi ndogo, na nitaenda kuchagua hiyo nafasi na ni bonyeze forward slash key.

Hii inaashiria moja kwa moja inachagua pengo. Kwa hivyo naweza kuijaza na yaliyomo kwenye clip yangu.

Juu ya source monitor nitaenda ku right click na nitachagua clear in na out, na nitachagua inpoint ambayo itafanya kazi vizuri kwangu na nitaenda kufanya overwrite edit.

Wakati huu muda umetajwa na in na outpoints kwenye sequence badala ya clip.
Na kwa sababu tunayo inpoint kwenye clip, imelingana na inpoint ndani ya sequence.
Tungekuwa na urahisi wa kuweka out point ndani ya clip badala yake na bila shaka yaliyomo kwenye clip ingerudishwa kwa wakati kujaza pengo hilo.

Hii ni njia moja powerful ya kufanya edit ndani ya premiere pro cc Ikiwa unahitaji kubadilisha yaliyomo au kujaza yaliyomo ambapo mwisho wa clip inajalisha zaidi ya mwanzo.

Kujua nini cha kutarajia wakati unaondoa moja au in ama outpoint inakupa udhibiti zaidi katika ku edit.

Inaweza kuwa ya utata wakati unapoanza . kwanza lakini njia bora ya kupata faida ni kujaribu mwenyewe.

Inafaa kuzingatia kuwa source patching buttons hubadilisha track ya clips itakayo ongezwa. Unaweza kuzivuta juu au chini kubadilisha hiyo.

Inafaa pia kuzingatia kwamba track selection buttons haina athari yoyote kwa three point edits.

Kwa hivyo hiyo ni utangulizi kwa three- point editing ndani ya adobe premiere pro cc.
Na asante sana kwa kutazama
Kwa mafunzo zaidi jiunge na kila siku ya wiki.

https://www.adobe.com/

Post Author: hatefull